JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Mkasa wa kimapenzi wa Shakira na mtoto wa Rais, Antonio

Mkasa wa kimapenzi wa Shakira na mtoto wa Rais, Antonio

Kabla ya Gerard Pique, Shakira alikuwa na mahusiano na Wakili kutoka Argentina, Antonio de la Rua tangu mwaka 2000 hadi Januari 2011 walipoachana rasmi.

Shakira Antonio

Antonio de la Rua ni mtoto wa Rais wa zamani wa Argentina, Fernando de la Rua ambaye aliongoza nchi hiyo kutoka mwaka 1999 hadi 2001, na alikuwa mshauri wa Baba yake kipindi cha Urais. Mama yake anaitwa Ines Pertine.

Shakira Antonio

Baada ya miaka 10 pamoja, Shakira na mume wake huyo walitengana hapo Agosti 2010 katika kile walichoeleza ni uamuzi wa pande zote mbili lakini Antonio ataendelea kusimamia biashara na masilahi ya kazi za sanaa za Shakira kama ambavyo amekuwa akifanya.

Soma pia Makala: Historia ya Aaliyah, muziki, filamu, skendo na R Kelly hadi kifo!

Mwimbaji huyo wa Hips Don’t Lie, kupitia tovuti wake, Januari 10, 2011 alitangaza rasmi kuachana kwao na Antonio na kile walichokubaliana kwa pamoja.

“Tangu Agosti 2010 tumekubaliana kwa pamoja kuchukua muda kuwa mbali na mahusiano yetu ya kimapenzi, katika wakati wote tumeendelea kufanya kazi pamoja, tumebakia kuwa karibu na kuweka faragha masuala yote,”.

Shakira

“Kwa pamoja tunakitazama kipindi hiki cha kutengana kama cha muda tu, na muda wa kila mmoja kukua huku tukiendelea kama washirika upande wa biashara,” alisomeka wakara huo wa mrembo huyu.

Download Music: Shakira – Hips Don’t Lie

Hata hivyo, Septemba 2012, Antonio alimshtaki Shakira kwa kudai fidia ya Dola100 milioni wastani wa Sh233.1 bilioni kwa kile alichodai alichangia sehemu kubwa ya mafaniko ya mwimbaji huyo. Lakini Agosti 2013 Mahakama ya Juu huko Los Angeles alitupilia mbali kesi hiyo.

Soma pia Makala: Mweleko mpya maisha ya Kanye West katika ndoa na Bianca Censori

Miongoni mwa dili ambazo Antonio alikuwa anadai kuzileta kwa Shakira ni ile na kampuni ya matamasha, Live Nation yenye thamani ya Dola300 milioni kwa kipindi cha miaka 10. Lakini kwa wakati wote Shakira alisema alifanya kazi na Antonio kama mshauri wake wa kibiashara na alilipwa kwa kazi hiyo.

Shakira and Antonio

Forbes Colombia iliripoti kuwa kufikia mwaka 2018, Shakira ndiye msanii wa kike wa Kilatini aliyeuzwa zaidi kwa wakati wote, anasifika kwa kufungua milango ya soko la kimataifa kwa wasanii wengine wa Kilatini.

Shakira ameshinda tuzo tatu za Grammy, tuzo 12 za Latin Grammy Awards, tuzo nne za MTV Video Music Awards, tuzo saba za Billboard Music Awards, tuzo 39 za Billboard Latin Music Awards, huku akiwa na rekodi sita za Guinness World Records.

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!