JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Kolabo tano kali za Darassa kwa muda wote

Kolabo tano kali za Darassa kwa muda wote

Huwezi kuzungumzia umaarufu wa muziki wa Darassa bila kutaja majina ya wasanii alioshirikiana nao (kolabo), anajua nani na kwa wakati gani akisikika katika wimbo wake, basi itakuwa ni bidhaa nzuri itakayouzika kwa urahisi kwa muda huo.

Ni njia aliyochagua kupita tangu awali, hata wimbo wake wa kwanza kurekodi ‘Kieleweke’ alimshirikisha Steve RnB, ni kabla ya kutoka na ‘Sikati Tamaa’ akiwa na Ben Pol, alijua historia ya muziki wake mbeleni itabebwa na kolabo kali atakazofanya.

Soma pia Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Jay Melody

Darassa, Mkurugenzi Mtendaji wa Classic Music Group (CMG) aliyepewa jina hilo na marehemu Complex, kwa miaka zaidi ya 10 ndani ya Bongofleva amefanikiwa kutengeneza ngoma kubwa ila nyingi zilizofanya vizuri ni zile alizoshirikisha wasanii wenzake.

Darassa kolabo

Ndivyo ilivyo kwa Darassa, asilimia kubwa ya nyimbo zenye historia, umaarufu na msisimko mkubwa kutoka kwake ni zile alizofanya kolabo na mastaa wengine wa Bongo na kimataifa, miongoni mwao ni hawa wafuatao;.

  1. Ben Pol

Ni wazi Ben Pol ndiye msanii pekee wa Bongofleva mwenye historia kubwa katika muziki wa Darassa, aliimba kiitikio cha wimbo wake, Sikati Tamaa (2012) uliomtoa kimuziki, ni ngoma iliyofanya vizuri hadi kuachia remix yake akiwa na Godzilla na Joh Makini.

Darassa kolabo

Ilimchukua Darassa miaka zaidi ya mitatu kutengeneza ngoma nyingine kubwa yenye hadhi kama ‘Sikati Tamaa’, nayo ni Muziki (2016) akimshirikisha Ben Pol tena. Hadi sasa hakuna ngoma ya Darassa iliyouza zaidi katika majukwaa ya kidigitali kama hii, huku ikimpatia dili nyingi.

Ikumbukwe video ya wimbo ‘Muziki’ inashikilia rekodi kama video ya msanii wa Rap au Hip Hop iliyotazamwa zaidi YouTube ikiwa na ‘views’ zaidi ya milioni 25, ikiwa imeipita video ya wimbo wa AY, Zigo Remix (2016) ft. Diamond Platnumz yenye ‘views’ milioni 20.

  1. Nandy & Marioo

Moja ya ngoma zilizompa Darassa heshima kubwa miaka ya hivi karibuni ni ‘Loyalty’ kutoka katika albamu yake ya kwanza, Slave Becomes a King (2020) akiwashirikisha wadogo zake kimuziki, Nandy na Marioo.

Darassa kolabo

Wimbo huu ndio ilimpatia tuzo yake ya kwanza kutoka tuzo za muziki (TMA) ambapo ulishinda kama Wimbo Bora wa Kushirikiana 2021 baada kuzibwaga nyimbo kama Ndombolo (Alikiba), Shikilia (Professor Jay), Unaua Vibe (Rapcha) na Lala (Jux).

Utakumbuka huu ulikuwa ni wimbo wa pili kwa Darassa kumshirikisha Marioo baada ya ule wa Chanda Chema (2019) uliomrudisha vizuri katika muziki baada ya ukimya mrefu wa tangu Agosti 2017 hadi Septemba 2018 kwa kile alichodai alikuwa kwenye mapumziko.

  1. Alikiba

Mafanikio ya albamu, Slave Becomes a King (2020) katika majukwaa ya kidigitali pindi ilipotoka tu kwa asilimia kubwa yalichochewa na ngoma ‘Proud of You’ ambayo Darassa alimshirikisha Alikiba kutokea Kings Music.

Darassa kolabo

Ni ngoma ambayo Darassa alijua itabeba albamu hiyo na ndio sababu katika orodha ya nyimbo 21 ndio namba moja na ndio ngoma ambayo video yake ilikuwa ya kwanza kuachiwa kutoka katika albamu hiyo kisha ikafuata Waiter, Loyalty na Size Yao.

Ikumbukwe mwaka 2020 albamu ya Darassa ‘Slave Becomes a King’ ndio ilikuwa albamu iliyotoka na nyimbo nyingi zaidi kwa mwaka huo zikiwa ni 21, huku ikifuatiwa na ya Harmonize, Afro East (18) na Story of The African Mob (12) ya Navy Kenzo.

  1. Sho Madjozi & Bien

Jicho lake akiwa Bongo akamuona Sho Madjozi wa Afrika Kusini na Bien kutokea kundi la Sauti Sol, Kenya, Darassa akajua kufanya kolabo nao ni biashara nzuri kwake na kwa asilimia kubwa amefanikiwa kufuatia na mapokezi ya nyimbo hizo.

Sho Madjozi amesikika katika wimbo, I Like It (2020) ambao ulibamba sana, video yake imefikisha ‘views’ zaidi ya milioni 13 ikiwa ni video ya pili ya Darassa iliyotazamwa zaidi huko YouTube kwa muda wote baada ya Muziki.

Kolabo yake na Bien, No Body (2023) ambayo bado inafanya vizuri, hadi sasa imesikilizwa (streams) zaidi mara milioni 14. 8 katika mtandao wa Boomplay na ndio wimbo wa kwanza wa Darassa kufikia mafanikio hayo. Hata albamu yote ya Slave Becomes a King hajafikia namba hizo.

Download Music: Darassa Ft. Bien – No Body

Utakumbuka Darassa ameshirikiana na wasanii wengine kama Jux (Leo, Juju), Maua Sama (Shika, Tumepoteza), Rich Mavoko (Kama Utanipenda, Segedance), Mr. Blue (Heya Haye), Wini (Nishike Mkono), Nay wa Mitego (Tunaishi), Harmonize (Yumba) n.k.

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!