JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Nilipenda uigizaji kabla ya muziki – Tiwa Savage

Nilipenda uigizaji kabla ya muziki – Tiwa Savage

Staa wa Afrobeats kutokea Nigeria, Tiwa Savage, 44, amesema katika kujitafuta katika tasnia ya burudani, alipenda sana uigizaji kabla ya muziki ambao umempatia umaarufu na mafanikio ya kiuchumi.

Tiwa Savage muziki

Kauli ya Tiwa Savage inakuja baada ya kucheza filamu mpya ‘Water and Garri’ ambayo inatarajiwa kutolewa kwenye Prime Videos mnamo Mei 10, 2024, huku akicheza kama muhusika mkuu.

Soma pia Rihanna afunguka anavyojivunia watoto wake

Mnamo Februari 2023, kupitia Instagram ndipo Savage alitangaza ujio wa filamu hiyo iliyoongozwa na Meji Alabi na kushirikisha waigizaji wengine kama Mike Afolarin, Andrew Bunting na Jemima Osunde.

Katika mahojiano na ABC hivi karibuni, Savage alijadili athari za kimataifa za muziki wa Afrobeats kwenye utamaduni wa Pop hadi kuja kuwa na ushawishi mkubwa duniani kote.

Tiwa Savage muziki

Kubwa zaidi Savage akabanisha kuwa mapenzi yake ya awali yalikuwa katika uigizaji na kuelezea furaha yake ya kurudi kwenye uwanja huo akiwa kama mtayarishaji mkuu akishirikiana na Vannessa Amadi-Ogbonna.

“Siku zote nilitaka kufanya uigizaji, siku zote nilitaka kufanya sinema. Kwa kweli, hilo ndilo lilikuwa chaguo langu la kwanza kabla ya muziki. Hatimaye nilihisi ni wakati sahihi kuingia huko, sikuwahi kutaka kuacha muziki, kwa hiyo ni njia nzuri kwangu kuendelea kuigiza,” alisema Tiwa Savage.

Savage ameandika na kutumbuiza wimbo wa filamu hiyo ambayo inasimulia kisa cha Aisha, mbunifu wa mitindo kutoka Marekani ambaye anarudi katika nchi yake ya asili kufuatia msiba wa familia.

“Utayarishaji mkuu ulikuwa kwa mimi kuvaa kofia ya Bosi wangu na kujaribu kuwa Boss Lady katika nyanja zote za maisha yangu. Ilikuwa ya kufurahisha na ilikuwa ya kufadhaisha kufanya hivyo.” alisema.

Tiwa Savage muziki

“Lakini ilinionyesha tu kwamba ninaweza kufanya chochote ninachoweka akilini mwangu. Kuna mambo mengi ambayo nina ndoto ya kuyatimiza na sasa nimehamasika sana.” alisema Savage.

Download Music: Zuchu – Zawadi

Akiwa na miaka 11 Savage alihamia London, Uingereza kwa ajili ya masomo, miaka mitano baadaye alianza kazi yake ya muziki akiimba nyimbo za wasanii kama vile George Michael na Mary J. Blige hadi alipokuja kuhitimu chuo cha muziki cha Berklee.

Mwaka 2012 alirejea Nigeria na kusaini Mavin Records inayomilikiwa na Don Jazzy na mwaka uliofuatia alitoa albamu yake ya kwanza, Once Upon a Time (2013) ikiwa na nyimbo kama ‘Kele Kele Love’ ambao ulivuma sana Afrika na kumtambulisha vizuri.  

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!