JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Amber Rose ataka Sh51 bilioni kwa Kanye West

Amber Rose ataka Sh51 bilioni kwa Kanye West

Mwanamitindo Amber Rose amesema kutokana na kuwa na mchango katika albamu ya aliyekuwa mpenzi wake, Kanye West, My Beautiful Dark Twisted Fantasy (2010) anastahili mgao wa Dola20 milioni, wastani wa Sh51 bilioni.

My Beautiful Dark Twisted Fantasy ni albamu ya tano ya Kanye West na ilitoka Novemba 2019 chini ya Def Jam Recordings na Roc-A-Fella Records, huku ikishirikisha wakali kama Jay Z, Rihanna, Nicki Minaj, Elton John, Rick Ross, John Legend nk.

Soma pia Namna mshindi wa tuzo za BET anavyopatikana

Albamu hiyo iliyoshika namba moja chati za Billboard 200 na kuingia 10 bora katika nchi tano tofauti, ilishinda tuzo za 54 za Grammy kama Abamu Bora ya Rapa, pia ilishinda tuzo za BET Hip Hop 2011.

Amber Rose Kanye West

Katika mahojiano na Jason Lee hivi karibuni, Amber Rose alipoulizwa kama alipata chochote kutoka katika wimbo, Monster (2010) ambao alichangia, alisema hakuna alichopata zaidi ya Nicki Minaj kumtaja katika wimbo huo.

“Nilipaswa kupata fedha kutokana na kazi hiyo kama Dola20 milioni ila sikupata chochote. Nilipaswa kulipwa kwa njia fulani kwa kutumia mfano wangu,” alisema Amber Rose ambaye alikuwa na uhusiano na Kanye hadi mwaka 2010.

Kauli ya Amber Rose inakuja mwaka mmoja baada ya Kanye West kuporomoka kutoka kwenye hadhi ya Ubilionea baada ya mgogoro wa kibishara kati yake na kampuni ya Adidas kufuatia matamshi yake ya chuki dhidi ya Wayahudi mwaka 2022.

Amber Rose Kanye West

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki katika mitandao ya kijamii wamemjia juu Amber Rose kwa madai kuwa hapaswi kumdai Kanye West kutokana ndiye alimfungulia dunia kwa kumpa umaarufu ambao yupo nao hadi leo ikimnuisha kwa mambo mengi.

Uhusiano wa wawili hao ulianza mwaka 2008 hadi 2010 walipoachana, kisha Kanye West kuwa na warembo wengine kama Julia Fox, Venetria, Kim Kardashian na mkewe wa sasa Bianca Censori ambaye walifunga ndoa ya faragha hapo Januari 2023.

Amber Rose Kanye West

Na kwa upande wake Amber Rose, tangu kuachana na Kanye West amehusishwa na wanaume wengine maarufu kama Machine Gun Kelly, 21 Savage, Odell Beckham Jr. na Wiz Khalifa ambaye aliolewa naye na kupata mtoto mmoja.

Ikumbukwe mnamo Februari 2023 Kanye West alipoteza hadhi ya Ubilionea baada ya Adidas kukatisha mkataba wao wa kibiashara uliozalisha bidha za viatu kupitia chapa yake,Yeezy. Kwa mujibu wa Forbes, utajiri wake uliporomoka kutoka Dola1.5 bilioni hadi Dola400 milioni.

Editor

Related Posts

Mocco Genius atoa nyota tano kwa Alikiba!

Mocco Genius atoa nyota tano kwa Alikiba!

Davido says Afrobeats is not his genre of music

Davido says Afrobeats is not his genre of music

Rayvanny X Iyanya & Zaba – Zazazela

Rayvanny X Iyanya & Zaba – Zazazela

Nilipenda uigizaji kabla ya muziki – Tiwa Savage

Nilipenda uigizaji kabla ya muziki – Tiwa Savage

error: Content is protected !!