JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Hamisa Mobetto anatisha kwa Mitindo, akomba tuzo kibao!

Hamisa Mobetto anatisha kwa Mitindo, akomba tuzo kibao!

Licha ya kuamua kuingia kwenye uingizaji na muziki, Hamisa Mobetto bado anaonekana kuwa na nyota nzuri zaidi upande wa mitindo kuliko kazi hizo nyingine hadi kushinda tuzo.

Hamisa Mobetto tuzo

Februari 2021 alipata tuzo kutoka Young C.E.O Round Table katika kipengele cha Fashion Icon ukiwa ni mwendelezo wa yeye kushinda na kutunukiwa tuzo kutokana na mitindo.

Soma pia Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Hamisa Mobetto

Hamisa ambaye ni C.E.O wa Mobetto Styles, maisha yake katika ulimwengu wa mitindo na urembo yamekuwa yakitawaliwa na tuzo na mataji.

Hamisa Mobetto tuzo

Utakumbuka Septemba mwaka 2021 Hamisa alishinda tuzo za Scream 2021 kutoka Nigeria ambazo hutolewa kwa vijana mbalimbali barani Afrika waliofanya vizuri kwenye sekta mbalimbali.

Download Music: Hamisa Mobetto – Madam Hero

Kwa nyakati tofauti Hamisa ameshinda na kuchaguliwa kuwania tuzo za Starqt zinazohusisha biashara, mitindo, michezo na burudani toka nchini Afrika Kusini.

Tuzo hizo zilizoanza mwaka 2014 kwa lengo kwa kuwatunuku Mastaa wa Afrika, Hamisa amewahi kushinda katika kipengele cha People Choice Awards.

Ikumbukwe jina la Hamisa Mobetto lilianza kuwa maarufu Bongo mara baada ya kutwaa taji la Miss XXL, After School Bash 2010, mashindano ya urembo yaliyoandaliwa na kipindi cha XXL kutoka Clouds FM.

Hamisa Mobetto tuzo

Hata hivyo, nyota yake ilianza kung’ara mwaka 2011 baada ya kuibuka mshindi wa pili Miss Dar Indian Ocean, pia mshindi wa pili Miss Kinondoni na kuingia nusu fainali ya Miss Tanzania.

Mwaka 2012 alishhiriki mashindano ya Miss University Africa na kuingia kwenye orodha ya Warembo 10 Bora.

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!