JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Mtangazaji wa Planet Bongo, Lesa aondoka East Africa Radio

Mtangazaji wa Planet Bongo, Lesa aondoka East Africa Radio

Mtangazaji wa kipindi maarufu cha burudani nchini, Planet Bongo kinachoruka East Africa Radio, Lesa ametangaza kuondoka katika kituo hicho baada ya kukitumikia kwa miaka mitano.

Lesa East Africa Radio

Ndani ya East Africa Radio Lesa alikuwa anaongoza show ya Planet Bongo kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, pamoja na Bongofleva Top 20 kila Jumamosi.

Soma pia Aaliyah arejea kwenye Utangazaji baada ya kuondoka Wasafi Media

Jana Aprili 12, 2024, Lesa kupitia ukurasa wake wa Instagram alitangaza kuondoka redio hiyo na kuwashukuru kwa kumpa nafasi ya kujifunza na kusisitiza bado wataendelea kuwa familia yake.

Lesa East Africa Radio

“Such a wonderful journey, 5 years nimekuwa hapa kujifunza na kukua ndio kitu ambacho, asante sana East Africa [Radio/TV].” aliandika Lesa na kuongeza.

“Ni kwaheri ila si ya kuonana maana sisi sio milima tutakutana marafiki na familia nilioipata hapo, ni kumbukumbu nzuri kwa popote nitakapokuwa.” alisema Lesa.

Kwa sasa Planet Bongo inayosikika kuanzia saa 01:00 mchana hadi 04:00 jioni, imebaki chini ya Rich Msafi na Piwa Magic ambaye alichukua nafasi ya Dullah Planet.

Mrembo huyu anakuwa Mtangazaji wa nne kuondoka katika show ya Planet Bongo ya East Africa Radio baada ya JR Junior, Frida Amani na Dullah Planet.

Download Music: Jay Melody – Nakupenda

Utakumbuka JR Junior kwa sasa yupo Times FM, Frida Amani ambaye anafanya muziki pia alijiunga na Clouds FM na Dullah aliyejiunga na Crown FM ya Staa wa Bongofleva, Alikiba.

Lesa East Africa Radio

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!