JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Diamond ni namba moja Tanzania katika mambo haya 10

Diamond ni namba moja Tanzania katika mambo haya 10

Mwimbaji wa Bongofleva toka WCB Wasafi, Diamond Platnumz amekuwa namba moja au msanii wa kwanza katika mambo haya 10 nchini Tanzania.

Diamond namba moja Tanzania

Diamond aliyetoka kimuziki mwaka 2009, tayari ametoa albamu tatu, Kamwambie (2010), Lala Salama (2012) na A Boy From Tandale (2018).

Soma pia Miaka mitano ya Zari kulipigania penzi la Diamond

Na haya ni mambo 10 ambayo Diamond ni namba moja au alikuwa wa kwanza kuyafanikisha katika tasnia ya muziki Tanzania;.

  1. Msanii mwenye tuzo nyingi

Kwa kipindi cha miaka 12 katika muziki wa Bongofleva, Diamond ameweza kushinda na kutunukiwa tuzo zaidi ya 46 za ndani na za kimataifa, huku akimpiku Lady Jaydee wenye tuzo zaidi ya 35.

Diamond namba moja Tanzania
  1. Msanii anayetazamwa zaidi YouTube

Sio Tanzania tu, bali katika nchi zote za Kusini mwa Jangwa la Sahara, huyu ndiye msanii aliyetazamwa zaidi YouTube katika ukanda huo akiwa na ‘views’ zaidi bilioni 2.18.

  1. Msanii anayemiliki vyombo vya habari

Mwaka 2018 alitambulika kama msanii wa kwanza katika eneo hilo baada ya kuanzisha Wasafi Radio na TV, anatajwa kuwa msanii wa pili barani Afrika kufanya hivyo baada ya Youssou N’Dour wa Senegal.

  1. Msanii aliyeshinda tuzo nyingi usiku mmoja

Anashikilia rekodi ya kushinda tuzo saba za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) 2014 kwa usiku mmoja, anakaribiwa na Alikiba aliyehinda tuzo tano mwaka 2015 ikiwa ni sawa, 20 Percent kwa mwaka 2011 na Zuchu mwaka 2023.

  1. Msanii mwenye wafuasi wengi mtandaoni

Katika mitandao mitatu maarufu ya kijamii Diamond ni namba moja kwa kujizolea wafuasi wengi, Instagram ana wafuasi milioni 16, Twitter milioni 1.3 na Facebook milioni 6.9.

Diamond namba moja Tanzania
  1. Msanii wa kwanza kuwania BET

Huyu ndiye msanii wa kwanza Bongo kuchaguliwa kuwania tuzo za kituo cha TV cha Black Entertainment Television (BET) katika kipengele Best International Act, tayari amewania mara tatu (2014, 2016 & 2021) na kumfanya kuwa msanii pekee aliyewania mara nyingi.

Download Music: Zuchu – Kwikwi

  1. Msanii mwenye video ghali zaidi

Video ya wimbo wake ‘Nana’ inatajwa kugharimu Dola40,000, wastani wa Sh92.7 milioni, hakuna msanii Bongo aliyewahi kusema amefanya video zaidi ya bei hiyo, anafuatiwa na Alikiba ambaye video ya ngoma yake ‘Aje’ iligharimu Dola32,000, wastani wa Sh74.2 milioni.

  1. Tuzo mbili MTV EMA

Hapo Oktoba 25, 2015 huko Milan, Italy, Diamond aliandika rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Afrika kushinda tuzo mbili za MTV EMA katika vipengele viwili kwa wakati mmoja.

  1. Anaongoza kwa subscribers YouTube

Diamond ndiye msanii mwenye ‘subscribers’ wengi zaidi YouTube Kusini mwa Jangwa la Sahara akiwa nao milioni 7.7 hadi sasa.

Diamond namba moja Tanzania
  1. Msanii wa kwanza kununua Rolls-Royce Cullinan

Julai 2022 Diamond alifanikiwa kulifikisha nchini gari la ndoto zake za muda mrefu, Rolls-Royce Cullinan ambalo amelinunua Dubai. Anaungana na wasanii wa Nigeria kama Davido na Burna Boy ambao nao mwaka huu amenunua gari la aina hiyo ambalo ni la kifahari.

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!