JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Honest Thief: Mwizi aliyethibiti wezi wenziye – film story & review!

Honest Thief: Mwizi aliyethibiti wezi wenziye – film story & review!

Honest Thief film; Mwanajeshi wa zamani wa Marekani, Liam Neeson ‘Tom Dolan’, amekuwa mwizi mkubwa na wa aina yake, mwizi mwenye busara za kipekee, ameiba kiasi kikubwa cha fedha lakini hazitumii kabisa!.

Honest Thief film

Tom anakutana na mrembo Kate Walsh ‘Annie Wilkins’ na kuvutiwa naye, huyu ni mwanafunzi aliyehitimu masomo ya saikolojia, anampa kazi katika kitengo chake cha kuhifadhi fedha zake. Katika mahusiano yao, Tom anawaeleza FBI kuhusu wizi wake ili ili aepuke kesi ya jinai.

Soma pia Day Shift: Biashara ya meno ya Vampire – film story & review!

Wakala wa FBI, Robert Patrick ‘Agent Sam Baker’ anawatuma wasaidizi wake, Jai Courtney ‘John Nivens’, na Anthony Ramos ‘Ramon Hall’ kuchunguza suala hilo.

Tom anawaelekeza sehemu alipohifadhi fedha hizo, lakini Nivens anamshawishi Hall kuziba na kwenda kuzifadhi sehemu nyingine.

Baada ya kuiba, Nivens na Hall wanarudi katika Hoteli anayoishi Tom, wanamtolea Bastola na kudai kuwa ana fedha nyingine nyingi kazificha sehemu.

Honest Thief film

Hata hivyo, ghafla Bosi wao, Baker anawasili hapo, katika majibizano, Nivens anamuua Baker, na Tom analazimika kukimbia ambapo nje anamkutana Annie na gari lake, kisha wanaondoka wote.

Tom anamwambia Annie kila kitu na anamshawishi atoroke akihofia usalama wake, lakini Annie anarudi kwenye kitengo cha kuhifadhi fedha kupata ushahidi wa kamera za usalama ambazo zinaonyesha Nivens na Hall wakiiba fedha.

Nivens na Hall wanajitokeza, Nivens anampiga Annie hadi kupoteza fahamu anafikiri amekufa, lengo la kufanya hivyo ni kupoteza ushahidi.

Tom anakuja na kumkimbiza Hospitali, kisha anaingia kwenye pambano lingine dhidi ya Polisi na rafiki wa Baker, Jeffrey Donovan ‘Sean Meyers’ ambaye pia ni wakala wa FBI lakini mwishoni anafanikiwa kuwatoroka.

Honest Thief film

Nivens anaenda Hospitalini ili kumuua Annie, lakini hawezi kumkaribia kwa sababu Meyers amekaa kwenye chumba chake ili akipona amtumie katika upelelezi.

Baadaye, Meyers anatambua kwamba Tom anasema ukweli baada ya kuona ripoti ya Nivens hairidhishi.

Tom anamvizia Hall nyumbani kwake na kumshawishi achane na picha za usalama za eneo la nyumba ambapo fedha zilihifadhiwa.

Naye Hall anamuonya Tom kuwa maisha ya Annie yako hatarini, baadaye Tom anamtorosha Annie Hospitalini na kumpeleka sehemu salama, huko anatengeneza vilipuzi ambavyo wanaenda kuilipua nyumba ya Nivens.

Kisha Tom anamtuma Annie kwenda kumpa Meyers picha za usalama na fedha zingine kutoka kwenye kitengo kingine cha uhifadhi kama kuonyesho uaminifu wake.

Film: Honest Thief
Director: Mark Williams.
Date: Oktoba 16, 2020

Editor

Related Posts

Red Notice: Wizi wa mayai ya Cleopatra watikisa – film story & review

Red Notice: Wizi wa mayai ya Cleopatra watikisa – film story & review

Outside the Wire: Vita itakayoibuka mwaka 2036 – film story & review

Outside the Wire: Vita itakayoibuka mwaka 2036 – film story & review

The Devil All the Time: Matendo kama ya Shetani – film story & review

The Devil All the Time: Matendo kama ya Shetani – film story & review

The Old Guard: Mishe ya watu wasiokufa! – film story & review

The Old Guard: Mishe ya watu wasiokufa! – film story & review

error: Content is protected !!