JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Mtu Mzee zaidi duniani afariki na miaka 118, ni Mtawa André

Mtu Mzee zaidi duniani afariki na miaka 118, ni Mtawa André

Mtu Mzee zaidi duniani na Mtawa wa Ufaransa, Lucile Randon ‘Sista André’ amefariki dunia hapo jana Januari 17, 2023 akiwa usingizini huko Toulon, Ufaransa, akiwa na umri wa miaka 118.

Mtu Mzee zaidi duniani

Kwa mujibu wa kitabu cha rekodi za dunia, Guinness, Sista André ndiye alikuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi wa kuishi duniani.

Soma pia Makala: Penzi la Alicia Keys latoa funzo kwa Zari na Hamisa

Sista André alizaliwa kusini mwa nchi ya Ufaransa mnamo Februari 11, 1904, wakati vita vya kwanza vya dunia vilipokuwa bado muongo mmoja kuanza.

Mtu Mzee zaidi duniani

Alitajwa kama Mzungu mzee zaidi duniani, kabla ya kifo cha Kane Tanaka wa Japani mwenye umri wa miaka 119 kufariki hapo Aprili 19, 2023.

Hivyo Randon kutambulila rasmi kama mtu aliyeishi kwa muda mrefu zaidi duniani.

Yeye ndiye mtu wa nne kwa umri mkubwa zaidi kuthibitishwa kuwahi kutokea, na pia mtu mzee zaidi aliyenusurika kwenye Covid-19 baada ya kupimwa mwezi mmoja kabla ya siku yake ya kuzaliwa ya 117.

Alilelewa katika familia ya Kiprotestanti akiwa msichana pekee kati ya ndugu watatu, wanaoishi katika mji wa kusini wa Ales. Mojawapo ya kumbukumbu zake nzuri ni kurudi kwa kaka zake wawili mwishoni mwa Vita vya Kwanza vya Kidunia.

Mtu Mzee zaidi duniani

Download Music: Harmonize – Nitaubeba

Akiwa kijana mdogo, Randon aligeukia Ukatoliki na kufanya kazi kama mlezi, mwalimu, mtawa, na mmisionari kabla ya kustaafu akiwa na umri wa miaka 75 mwaka 1979.

Aliishi katika makao ya wazee huko Toulon, Ufaransa kuanzia mwaka 2009 hadi kifo chake.

Editor

Related Posts

Mtangazaji Gardner G. Habash afariki dunia

Mtangazaji Gardner G. Habash afariki dunia

Aliyecheza ‘The Gods Must Be Crazy’ adai kutolipwa kwa miaka 34

Aliyecheza ‘The Gods Must Be Crazy’ adai kutolipwa kwa miaka 34

Wasanii wasiotumia mitandao ya kijamii

Wasanii wasiotumia mitandao ya kijamii

Hatari za kukaa bila kufanya mazoezi

Hatari za kukaa bila kufanya mazoezi

error: Content is protected !!