JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Aliyecheza ‘The Gods Must Be Crazy’ adai kutolipwa kwa miaka 34

Aliyecheza ‘The Gods Must Be Crazy’ adai kutolipwa kwa miaka 34

Kuna mengi ya kushangaza, moja wapo ni hili la Staa wa filamu kutokea nchini Namibia,  Leonora Jacobs ambaye anadai kutolipwa chochote tangu acheze filamu, The Gods Must Be Crazy II zaidi ya miaka 34 iliyopita.

The Gods Must Be Crazy

Leonora, 42, akiwa na umri wa miaka mitano alicheza filamu, The Gods Must Be Crazy II (1989) iliyokutanisha waigizaji wengi maarufu Sahara Kusini ikiwemo N!xau Toma maarufu kama ‘Bushmen’ kutokea Namibia.  

Soma pia Somo kutoka kwa binadamu mweusi zaidi duniani

The Gods Must Be Crazy II ni filamu ya vichekesho iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa kimataifa kati ya Afrika Kusini, Botswana na Marekani, huku kampuni ya Weintraub Entertainment Group wakisimama kama watengenezaji.

The Gods Must Be Crazy

Akizungumza katika video iliyosambaa mtandaoni, Leonora anadai kuwa walimwahidi kwamba akifikisha umri miaka 21 watamlipa kwa kucheza nafasi yake lakini hadi sasa hajapokea hata senti kutoka kwa kampuni ya uzalishaji.

“Mimi ni miongoni mwa waigizaji waliocheza filamu hiyo, kipindi hicho nikiwa na umri wa miaka mitano tu na sasa nina miaka 42, sehemu niliyoshiriki ni pale ambapo nilicheza na fisi,” alisema na kuongeza.

“Nafikiri nilitakiwa kupata chochote kitu kutokana ile ni kazi yangu niliyofanya kwenye uhusika wangu, hata hivyo hadi sasa sijapata chochote kitu, walituahidi nikifikisha umri wa miaka 21 watanilipa fedha zangu ila hadi leo hawajafanya hivyo,” alisema Leonora.

The Gods Must Be Crazy

Filamu The Gods Must Be Crazy II ilyoachiwa rasmi Oktoba 13, 1989 na 20 Century Fox, hadi sasa inakadiriwa kuuza zaidi ya Dola6.3 milioni, wastani wa Sh14.8 bilioni.

Muigizaji mwingine wa filamu hiyo, N!xau Toma inaelezwa alilipwa Dola300 wakati huo, wastani wa Sh709,000 kwa sasa.

Hata hivyo, Mkurugeni wa The Gods Must Be Crazy II, Jamie Uys alidai muigizaji huyo hakuwa anatambua umuhimu wa fedha na kuona kama karatasi, hivyo aliachana nazo!.

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!