JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

The Devil All the Time: Matendo kama ya Shetani – film story & review

The Devil All the Time: Matendo kama ya Shetani – film story & review

The Devil All the Time: Matendo kama ya Shetani – film story & review; Wakati wa vita vya pili vya dunia, akihudumu katika visiwa vya Solomon, Mjini Marine, Willard Russell anamkuta Miller Jones akiwa amechunwa ngozi na kutundikwa msalabani na Wanajeshi wa Japan.

The Devil All the Time

Ili asiendelee kuteseka, Willard anaamua kumpiga risasi Jones nyuma ya sikio kisha kufa.

Baada ya vita, akielekea nyumbani kwake huko Coal Creek, West Virginia, Willard anapitia Meade, Ohio ambapo anakutana na Haley Bennett ‘Charlotte’ ambaye ni Mhudumu katika Mgahawa.

Soma pia The Old Guard: Mishe ya watu wasiokufa – film story & review

Kitambo kidogo Willard na Charlotte wanaoana na kuhamia Knockemstiff, Ohio, ambapo wanajaliwa mtoto wa kiume na kumpa jina la Arvin Eugene Russell.

Mwaka 1950, Helen Hatton anaolewa na Roy Laferty ambaye ni Mhubiri mwenye matendo ya ajabu ingawa ni kivutio kwa baadhi ya waumini wake. Kwake ni kawaida kumuweka buibui wenye sumu kichwani kwake wakati akitoa mahubiri, lengo la kufanya hivyo ni kuonyesha imani yake kwa Mungu.

Helen na Roy wana binti anayeitwa Lenora Laferty, wakati wa Mahubiri, Roy anaumwa na buibui usoni mwake na kumletea athari kubwa.

Baadaye anakuja kuamini kwamba ana uwezo wa kufufua wafu, hivyo anamchukua Helen kwenda msituni ambapo anamchoma na bisibisi shingoni na kufa, kisha anajaribu kumfufua lakini anashindwa.

The Devil All the Time

Akirudi nyumbani Roy anapanda gari la wanandoa wawili, Carl Henderson na Sandy Henderson ambao huonyeshwa wauaji, lakini Carl ni binadamu wa ajabu sana, huwalazimisha watu kufanya mapenzi mkewe huko yeye akiwapiga picha, Roy anakataa kufanya mapenzi na Sandy, kwa hivyo Carl anampiga risasi na kumuua.

Soma pia The Devil of All Time: Matendo kama ya Shetani – film story & review

Mwaka 1957, Charlotte anagundulika kuwa na saratani, Willard anaamini anaweza kumshawishi Mungu kwa sala ya bidii kuondoa saratani kwenye mwili wa mkewe, huku akitoa dhabihu mbwa wa Arvin na kupiga magoti mbele ya msalaba wa Rustic ambao alikuwa ameuweka msituni nyuma ya nyumba yake, licha ya juhudi hizo Charlotte anafariki, hilo linapelekea Willard kujiua kwa kujikata koo.

Arvin, sasa ni yatima, anaenda kuishi na bibi yake Kristin Griffith ‘Emma’, ​​ambapo anakutana na Lenora, ambaye anakuwa dada yake wa kambo. Wanaelewana sana.

Mwaka 1965, Arvin anapewa bastola (Luger) ya baba yake kama zawadi ya siku ya kuzaliwa kwake, anamlinda sana Lenora ambaye kwa sasa anamezewa mate na wavulana wengi mtaani kwao.

Lenora anajenga ukaribu na Mchungaji Preston Teagarden ambaye ni mpya katika kanisa lao, Mchungaji Preston anamtongoza Lenora, wanaanzisha mahusiano hadi Lenora kubeba ujauzito.

The Devil All the Time

Hata hivyo, Mchungaji Preston anakataa ujauzito huo ili kutoleta aibu mbele ya kanisa na familia yake.

Lenora anaamua kujinyonga na kufa, baada ya uchunguzi, Arvin anaambiwa kwamba Lenora alikuwa mjamzito, anashuku kwamba Mchungaji Preston ndiye alikuwa muhusika.

Anamfuata Mchungaji Preston na kumuona akimtongoza msichana mwingine, wakiwa wawili pekee ndani ya kanisa, Arvin anamueleza Mchungaji Preston makosa yake, kisha anampiga risasi na kumuua.

Baadaye Arvin hupanda gari la wale wanandoa, Carl na Sandy, lakini anatambua kuwa Carl amebeba bunduki. Wakati Carl anajiandaa na ibada yake ya ajabu ya kulazimisha watu kufanya mapenzi na mkewe, Arvin anawapiga risasi na kuwaua wote wawili (Carl na Sandy) kwa kujilinda.

Katika chumba kupaki gari, ndugu wa Sandy, Lee anapata filamu na kuelewa kisa cha mauaji ya Sandy. Ili kujilinda na uchunguzi, anaenda kwenye nyumba ya Carl na Sandy ambapo anapata zile picha alizopiga Carl na kuziharibu.

The Devil All the Time

Arvin anasafiri kwenda Meade kutembelea nyumba yake ya utotoni, Lee anajua kwamba Arvin alimuua Mchungaji Preston, hivuo anamfuata huko Meade akiwa na bunduki.

Soma pia Marry Me: Jennifer Lopez agoma kufunga ndoa na Maluma – film story & review

Arvin yupo msituni kwenye msalaba wa Willard, anaibukiwa na Lee ambaye anataka kumuua, lakini Arvin anamuwahi na kumpiga risasi.

Kabla hajafa, Arvin anamuonyesha picha ya Sandy na maiti ya Roy, Arvin anaziachia picha na filamu ili kutoa ushahidi wa mauaji ya Carl na Sandy. Arvin anapanda gari na kuondoka zake.

Filamu: The Devil All the Time
Tarehe: September 11, 2020
Director: Antonio Campos

Editor

Related Posts

Red Notice: Wizi wa mayai ya Cleopatra watikisa – film story & review

Red Notice: Wizi wa mayai ya Cleopatra watikisa – film story & review

Honest Thief: Mwizi aliyethibiti wezi wenziye – film story & review!

Honest Thief: Mwizi aliyethibiti wezi wenziye – film story & review!

Outside the Wire: Vita itakayoibuka mwaka 2036 – film story & review

Outside the Wire: Vita itakayoibuka mwaka 2036 – film story & review

The Old Guard: Mishe ya watu wasiokufa! – film story & review

The Old Guard: Mishe ya watu wasiokufa! – film story & review

error: Content is protected !!