JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Namna Diamond Platnumz anavyovuna mamilioni ya fedha YouTube

Namna Diamond Platnumz anavyovuna mamilioni ya fedha YouTube

Baada ya kuwepo mjadala mkubwa unaodai msanii kufanikiwa upande wa YouTube sio kipimo cha ukubwa wa muziki wake, msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz ambaye ana mafanikio makubwa upande huo amemua kufunguka vilivyo.

Diamond YouTube

Diamond amesema msanii anapojivunia kutazamwa zaidi (views) YouTube, ni kwamba amefanikiwa kimauzo katika mtandao na sio majivuno yasio na tija, ingawa hilo pia litategemea wanaonunua kazi za msanii husika wanatokea nchi gani.

Soma pia Diamond anaingiza Sh120 milioni kwa mwezi kupitia YouTube!

Kauli ya Diamond imekuja kufauatia Mkurugenzi wa E FM na TV E, Francis Ciza ‘Majizzo’ kudai msanii kutazamwa zaidi YouTube haina uhusiano wa moja kwa moja na ukubwa wa muziki wake au jina lake.

Katika kile Diamond alichoita ni kutoa somo, alianza kutolea ufafanuzi baadhi ya maneno ambayo wamekuwa wakiyatumia katika biashara hiyo ya kuuza muziki mtandaoni.

Kwanza ni neno ‘streams’ maana yake mauzo kwa njia ya kusikiliza, pili ‘views’ maana yake mauzo kwa njia ya kutazama, tatu ‘downloads’ maana yake mauzo kwa njia ya mtu kupakua.

“Tanzania platform inayopendwa kutumiwa na wanunuzi wetu wa muziki ni YouTube na mauzo yao yanaitwa views. Hivyo mkisikia views tafsiri yake ni mauzo. Si ujivuni tu wa watu kutazama wimbo au content, ni distribution sales, mauzo kwa njia ya watu kutazama,” anasema Diamond.

Diamond anatolea mfano video ya wimbo wake ‘Waah’ alioshirikiana na Koffi Olomide kutoka DR Congo kwa kueleza ulipofikisha views Milioni 39.3 ulitengeneza Euro 32,266. Hadi kufikia sasa video ya wimbo huo tayari ina views zaidi ya Milioni 155 ikiwa ni miaka mitatu tangu itoke.

Diamond YouTube

“Sio kila wimbo ukifikisha views hizo unaweza kufikisha kiasi hicho cha pesa pia, unategemea wimbo huo umetazamwa kwenye nchini zipi, kwa sababu baadhi ya nchi views zake haziingiza kiasi kikubwa cha fedha,” anasema na kuongeza.

“Nchi zilizoendelea views zake zina kiasi kikubwa cha fedha kwa sababu waweka matangazo wanaweka bajeti kubwa, hivyo tujitahidi kuhakikisha kazi zetu zinafuatiliwa na watu wa nchi za nje,” anasema Diamond.

Pia ameeleza masanii anapojivunia video ya wimbo wake kuingia ‘trending’ upande wa YouTube sio jambo la kubezwa bali anastahili kupongezwa kwani ni ishara kuwa ubunifu wake umekubalika na watu.

Ikumbukwe kipindi cha nyuma msanii Harmonize aliwahi kuponda vilivyo kwa madai muziki wa Bongofleva anadumaa kwa wasanii kushindana kushika namba moja ‘trend’ YouTube, hivyo akaiomba serikali kuleta Tuzo za muziki ili wasanii washindane upande huo.

“Trending maana yake ni zinazovuma, ili kivume kinatakiwa kiwavutie watu kutaka kukifuatilia kwa kukitazama au kukisiliza, na kama kijana jukumu liko mikononi mwako. Ni eidha ubuni ujinga ili watu wafuatilie au ubuni kazi ili inapovuma ikuingizie kipato zaidi,” anasema Diamond.

“Ukiona kijana kaamua kubuni kazi na ikavuma ujue basi anapaswa kupongezwa, kuheshimiwa na kusapotiwa zaidi ili awe mfano bora na wengine nao wabuni kazi kwa sababu aliamua kuwaza chanya kwa maslai ya Taifa, maana angeweza kuweka video za utupu pia tena akavuma kiurahisi na kulitia aibu Taifa,” alisema Diamond.

Hadi sasa Diamond anaongoza katika nchini za Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kuwa na wafuatiliaji (Subscribers) wengi kwenye mtandao wa YouTube akiwa nao zaidi ya milioni 8.7. Vilevile ana rekodi ya kuwa msanii wa kwanza ukanda huo kwa kuweza kupata views Bilioni 1 tangu ajiunge na mtandao huo ulioanzishwa Februari 14, 2005 California nchini Marekani.

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!