JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Young Lunya

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Young Lunya

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Young Lunya; Ni miongoni mwa wasanii wa Hip Hop wenye ushawishi mkubwa sokoni kwa sasa, miaka ya hivi karibuni jina lake limechomoza kwenye kolabo nyingi kubwa za wasanii kama Harmonize na Professor Jay.

Young Lunya mambo 10

Ukali wake umemuwezesha kushinda tuzo mbili za muziki Tanzania (TMA) 2021 na kupata dili la kusainiwa RockStar Africa na Sony Music akiwa msanii wa kwanza wa Hip Hop Bongo. Huyu ndiye Young Lunya;.

Na haya ni Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Young Lunya

1.Mwanzo Young Lunya alikuwa anapenda kucheza mpira wa kikapu, sasa huko kwenye kikapu ndipo akakutana na watu wa Hip Hop na kuvutiwa na aina ya muziki huo, punde tu naye akajifunza kuchana na kuandika mashairi yake.

2.Young Lunya aliwahi kufanya muziki katika kituo cha Mkubwa na Wanawe kilichowatoa wakali kibao Bongo kama kundi la Yamoto Band, ila baada ya muda akaendelea na harakati zake nyingine hadi alipokuja kutoka.

Young Lunya mambo 10

3.Hata kundi la Mabantu nao walikuwepo katika kituo hicho, hivyo anapoona sasa Mabantu wamemshirikisha Lunya katika nyimbo zao tatu, No Love No Stress Remix (2020), Sponsa (2020) na Nawekera (2020), tambua wamefahamiana kitambo.

4.Baadaye Lunya alikuja kukutana na wenzake wawili, Salmin Swaggz na Conboi na kuunda kundi la OMG, Prodyuza Luffa ndiye aliwaweka pamoja na kuanza kufanya pale Switch Records walipotoka na wimbo wao, Uongo na Umbea (2017).

5.Quick Rocka ndiye aliyewapa OMG (Ooh My God) jina hilo baada ya kuona uwezo wao ni mkubwa, na hawa ndio wasanii wa kwanza kuwasaini katika lebo yake, Switch Music Group (SMG). Awali Quick Rocka alimpa Lunya jina hilo ila hakuwa tayari kulitumia.

6.Utakumbuka Quick Rocka ambaye aliunda kundi la Rockaz na wenzake watatu, Chief Rocka, Dau Rocka na Mo Rocka, nao walipewa jina hilo la Rockaz, Marehemu Albert Mangwair kufuatia kuridhika na uwezo wao.

Young Lunya mambo 10

7.Vesi aliyochana Lunya katika mdundo wa wimbo wa Ommy Dimpoz, Kata (2020), ndio ilimshawishi Seven Mosha ambaye ni Msimamizi wa Masoko na Maendeleo ya Wasanii Afrika Mashariki chini ya Sony Music Entertainment kumsaini katika lebo hiyo.

Na sasa yupo Sony Music pamoja na mastaa wengine wa Bongofleva kama Ommy Dimpoz, Abigail Chams na Aslay.

8.Wimbo wake, Mbuzi (2021) ni moja ya nyimbo za Lunya zenye historia kubwa kwake, ndio wimbo uliomuwezesha kushinda tuzo ya kwanza ya TMA, kupitia wimbo huo alishinda tuzo mbili kama Msanii Bora wa Kiume wa Hip Hop na Wimbo Bora wa Hip Hop.

Download Music: Young Lunya – Mbuzi

9.Sababu ya Young Lunya kujiita Mbuzi, yaani (G.O.A.T) akimaanisha the Greatest of All Time (Bora wa Muda Wote), ni kutokana na kuutumikia muziki kwa miaka zaidi 10 katika bora ule ule alioanza nao mwanzo.

10.Hata hivyo, Lunya sio msanii wa kwanza Bongo kujipa jina la Mnyama, kuna Fid Q (Mzee Mbuzi), Mr. Blue (Nyani Mzee), Diamond Platnumz (Simba), Harmonize (Tembo), Rayvanny (Chui), Country Boy (Fisi), Dudu Baya (Mamba), Afande Sele (Simba Dume) n.k.

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!