JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Rihanna afunguka anavyojivunia watoto wake

Rihanna afunguka anavyojivunia watoto wake

Mwimbaji wa Pop, Rihanna ambaye ni nguli wa muziki na urembo akiongea na Entertainment Tonight kwenye zulia jekundu, amefunguka jinsi anavyovutiwa na maisha ya watoto wake.

Rihanna watoto

Rihanna alivuma duniani kufuatia kuachia albamu yake ya tatu, Good Girl Gone Bad (2007), iliyokuwa na nyimbo kali kama Rehab, Hate That I Love You na Umbrella ambao ndio ulimpatia tuzo ya kwanza ya Grammy.

Soma pia Picha: Rihanna amuonyesha mtoto wake na A$AP Rocky

“Unajua nini? watoto wangu, wanaishi maisha makubwa zaidi. Upendo walionao kutoka kwa kila mtu, wanajua wanapendwa. Ninafurahi kuiona machoni mwao, nikijua kwamba kila mtu katika nyumba hii yuko karibu nao.” alisema.

Rihanna alikuwa mama kwa mara ya kwanza baada ya kuzaliwa kwa RZA mnamo Mei 2022, kisha, mnamo Agosti 2023, alimkaribisha Riot Rose. Amezaa watoto hao na Rapa ASAP Rocky, hitmaker wa wimbo, Needed Me.

Rihanna watoto

Licha ya kuongezeka kwa matarajio ya albamu yake ijayo, Rihanna ameonekana kutokuwa na presha ya jambo hilo na kuendelea kutumia muda wake zaidi na familia yake.

Katika mahojiano na Jarida la Interview Magazine mapema mwezi huu, Rihanna, hitmaker wa wimbo, Diamonds, alisema yuko tayari kupata watoto zaidi.

“Sijui Mungu anataka nini, lakini ningependa kuwa na watoto zaidi ya wawili. Nijaribu kupata msichana wangu, lakini bila shaka akiwa ni mvulana mwingine, basi ni mvulana wangu mwingine.” alisema Rihanna.

Hata hivyo, Machi mwaka huu Rihanna akiongea na Vogue China alisema ni jambo zuri zaidi kwake kulea wavulana hao wawili na amekuwa akiwapa muongozo sahihi.

“Watoto wanakuja ulimwenguni wakiwa na utu wao binafsi (asili) na uaminifu, bila mantiki yoyote au upatanifu, ambao kwa kawaida hukufanya uhisi kwamba lazima ujumuike katika kundi fulani.” alisema.

Rihanna watoto

“Inapendeza sana kuona, na ninataka kuendelea kuwasaidia na kuhakikisha kwamba wanajua wanaweza kuwa yeyote wanayetaka kuwa. Wanapaswa kuikumbatia kabisa hiyo kwa sababu ni nzuri na ya kipekee. Nawapenda hivyo hivyo.” alisema Rihanna.

Rihanna na A$AP Rocky walithibitisha uhusiano wao mnamo Novemba 2020 wakiwa visiwa vya Barbados, eneo ambalo wote wanatokea.

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!