JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Hamisa Mobetto

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Hamisa Mobetto

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Hamisa Mobetto; Tangu akiwa mdogo Hamisa Mobetto anakiri alipenda sana kuwa Mwanamuziki ila kutokana na kutafuta fedha akajikuta ameingia kwenye filamu na mitindo ambapo amepata mafanikio makubwa hadi kushinda tuzo kabla ya kuingia kwenye muziki.

Mambo 10 Hamisa Mobetto

Huyu ni Miss XXL After School Bash (2010), ni mshindi wa pili  wa Miss Dar Indian Ocean (2011), pia aliwahi kuingia nusu fainali ya Miss Tanzania (2011) na 10 bora ya Miss University Africa (2012). Na haya ni Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Hamisa Mobetto;

Soma pia Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Lady Jaydee

1.Katika wimbo wa Diamond Platnumz uitwao Nikifa Kesho kuna sauti ya Hamisa Mobetto ingawa hajatajwa kushiriki, hiyo ni sawa na Nandy na Ruby katika wimbo wa Christian Bella, Ollah.

2.Urafiki wa Hamisa Mobetto na Lira Garole ulianzia kwenye mtandao wa Instagram kwa kutumia Direct Message (DM), Lira aliwahi kuwa mpenzi wa msanii toka Marekani, Chris Brown, pia alionekana kwenye video ya wimbo wa Rick Ross na Chris Brown, Sorry.

Mambo 10 Hamisa Mobetto

3.Wimbo wa Hamisa, Madam Hero umeandikwa na msanii Foby na Prodyuza C 9, utakumbuka Foby ndiye amehusika kwenye kuandika na kutunga melody za wimbo wa Dayna Nyange, Komela.

Download Music: Hamisa Mobetto – Ex wangu Remix Ft Seneta Kilaka

4.Sauti ya kike inayosikika kwenye wimbo ‘Jibebe’ wake Diamond Platnumz, Lava Lava na Mbosso ni yake Hamisa, yaani yule anayeitikia ‘I like’ ni Hamisa. Huu unakuwa wimbo wa pili wa Diamond ambao Hamisa kaingiza sauti (back vocal) bila kutajwa kama amehusika.

5.Wengi wanajua kuwa wimbo wa kwanza Hamisa Mobetto kurekodi ni Madam Hero kutokana ndio wa kwanza kuachiwa toka kwake, hata hivyo, Hamisa alianza kurekodi wimbo uitwao Furaha bado haujatoka hadi sasa.

6.Mwaka 2021 Hamisa alitambulisha Lebo yake, Mobetto Music na kuwa msanii wa pili wa kike Bongo kutumia jina la familia upande wa lebo, wa kwanza ni Vanessa Mdee ambaye lebo yake imeipa jina la Mdee Music.

Soma pia Video 10 za bei ghali zilizowahi kufanyika Bongo

7.Hamisa alikuwepo wakati Tanasha anashuti video ya wimbo wa Alikiba, Nagharamia, ikumbukwe Tanasha na Hamisa wamezaa na Diamond lakini wakati huo wote bado walikuwa hawana mahusiano na Diamond.

8.Hamisa ndiye msanii wa kike kutoka kwenye Bongofleva anayeongoza kuwa na wafuasi (followers) wengi Instagram akiwa nao zaidi milioni 10.3 akiwa amempita Shilole ambaye sasa anashika nafasi ya pili akiwa na milioni 9.8.

Soma pia Mambo 10 usiyoyajua kuhusu G Nako

Mambo 10 Hamisa Mobetto

9.Hamisa ni shabiki mkubwa wa Mwana FA na wimbo aliyoanza kuupenda kutoka kwa Rapa huyo unaitwa Kama Zamani uliotoka Mei 2013 akiwashirikisha Kilimanjaro Banda (Njenje), Mandojo na Domo Kaya.

10.Ili Hamisa aweza kutokea kwenye video ya msanii ni lazima yeye ndiye awe muhusika mkuu (main character), utakumbuka tayari ametokea kwenye video kama Dodo ya Alikiba ambaye hadi anafika Zanzibar kwa ajili ya kushuti hakujua kama Hamisa atatokea kwenye video hiyo, ni jambo lilopangwa na uongozi wa Kings Music.

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!