JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Yanga, Simba zatupwa nje CAFCL 2023/24

Yanga, Simba zatupwa nje CAFCL 2023/24

Timu kutokea Tanzania, Yanga SC na Simba SC zimeondoshwa katika michuano ya klabu bingwa Afrika (CAFCL) 2023/24 katika hatua ya robo fainali.

Utakumbuka hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuingiza timu mbili robo fainali lakini zote zimeshindwa kufuzu kwenda nusu fainali.

Soma pia Sababu nne kwanini Arsenal inaweza kubeba UEFA

Mchezo wa kwanza hii leo Aprili 5, 2024 ulipigwa nchini Afrika Kusini ambapo Yanga walikuwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns, hadi dakika 90 zinaishi matokeo yalikuwa 0-0 kama ilivyokuwa mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Tanzania.

Yanga Simba CAFCL

Katika mikwaju ya penaliti Mamelodi walifunga 3, huku Yanga wakifunga 2. Penalti za Yanga zimefungwa na Augustine Okra na Joseph Guede, huku waliokosa wakiwa ni Aziz Ki, Dickson Job na Ibrahim ‘Bacca’ Hamad.

Kule Misri, Simba walipoteza goli 2-0 dhidi ya Al Ahly FC, utakumbuka katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Mkapa walishinda goli 1-0.

Yanga Simba CAFCL

Kwa matokeo hayo, Al Ahly ambayo ni mara ya kwanza kucheza na Simba hatua ya mtoano CAFCL, wanatinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa goli 3-0.

Download Music: Whozu Ft Mbosso & Billnass – Ameyatimba Remix

Ikumbukwe hii ni mara ya kwanza kwa Simba kupoteza michezo yote miwili ya nyumbani na ugenini dhidi ya Al Ahly katika michuano ya klabu bingwa Afrika (CAFCL).

Editor

Related Posts

Mbappe atangaza kuondoka PSG, kutua Real Madrid?

Mbappe atangaza kuondoka PSG, kutua Real Madrid?

Chama kuikosa Azam FC

Chama kuikosa Azam FC

Harry Kane atuma salamu kwa Real Madrid

Harry Kane atuma salamu kwa Real Madrid

Yanga SC 2-1 Simba SC: Aziz Ki aendeleza ubabe

Yanga SC 2-1 Simba SC: Aziz Ki aendeleza ubabe

error: Content is protected !!