JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Ndoa 10 za Mastaa Bongo zilizokufa kifo cha mende!

Ndoa 10 za Mastaa Bongo zilizokufa kifo cha mende!

Ndoa 10 za Mastaa Bongo zilizokufa kifo cha mende!; Kwa kawaida ndoa za watu maarufu duniani kote huteka hisia za wengi pindi zinapofungwa, wengi hupenda kufuatilia ndoa hizo kwa lengo la kujifunza na kupata hamasa mpya zaidi katika mahusiano yao.

Nchi Tanzania ndoa za wasanii wa filamu na muziki zimekuwa zikikodolewa macho na wengi, kubwa zaidi pale zinapovunjika huteka mazungumo kila kona.

Soma pia Wasanii 10 waliowahi kuwa na uhusiano na Mameneja wao!

Makala haya yanaenda kuangazia ndoa 10 za Mastaa Bongo zilifungwa miaka ya nyuma na sasa hazipo tena katika uso wa dunia;.

  1. Lady Jaydee

Ndoa ya Lady Jaydee na Mtangazaji wa kituo cha redio, Clouds FM, Gardner G Habash ilidumu kwa zaidi ya miaka 10, licha ya kuwa wanandoa, Gardner pia alikuwa akimsimamia Jide kimuziki.

Ndoa Mastaa Bongo

Walifunga ndoa Mei 2005 na ilipofika Desemba 2016 ndipo ilipotoka talaka rasmi na ukawa mwisho wa ndoa yao iliyovutia wengi tangu kufungwa kwake.

Lady Jaydee anaeleza aliamua kuomba talaka baada ya kuona imetosha, yaani ndoa yao haiwezi kuendelea tena, licha ya kuachana kwao, kwa sasa ni marafiki wanaoweza kukutana sehemu na kupiga stori na kunywa.

  1. Aunty Ezekiel

Msanii huyu maarufu wa Bongo Movie, alifunga ndoa Julai 2012 na mchumba wake ajulikanaye kama Sunday (Demonte) Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).

Ndoa hii ilisambaratika pale Sunday alipofungwa Dubai kwa kesi ya dawa za kulevya, Aunty alisema hakuachana na mume wake huyo wa ndoa lakini hawezi kurudiana naye tena kwa kuwa tayari kwa sasa ameshaanza maisha mengine.

Ni kweli maisha mengine!, mrembo huyo alianzisha mahusiano na dansa wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo na kufanikiwa kupata mtoto mmoja na baada ya hapo penzi lao likasambaratika, kisha Aunty kuwa Kusah na tayari wana mtoto.

  1. Alikiba

Kwa mujibu wa ujumbe wa mke wa Alikiba, Aminah aliotoa Instagram, Juni 15, 2023, ndoa hii haipo tena, Aminah anadai amekuwa akipambana ili Alikiba asaini talaka yake ili mwimbaji huyo amekuwa akimzungusha huku yeye akiendelea na maisha yake.

Ndoa Mastaa Bongo

“Nimeondoka katika maisha yako kuepuka maumivu na mateso mengi. Lakini mpaka Leo hutaki kunipa talaka huku wewe ukiwa huru kufanya mambo yako na mimi ukinifunga kwenye kivuli cha mke wa mtu,” alisema Aminah!.

Utakumbuka wawili hao walifunga ndoa Aprili 2018 Mombasa na baadaye wakafanya harusi kubwa Serena Hotel, Dar es Salaam, huku sherehe hiyo ikiweka rekodi ya kurushwa Mubashara Azam TV.

  1. Nuh Mziwanda

Mwimbaji huyu alifunga ndoa kimya kimya na mrembo aitwaye Nawal Novemba 2016 ikiwa ni miezi kadhaa tangu kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Shilole.

Hata hivyo, ilipofika Julai 2017 taarifa za kuachana kwao zilichukua nafasi wakiwa tayari wamejaliwa kupata mtoto mmoja, hivyo ndoa yao ilidumu kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja.

Download Music: Stamina Ft Atan – ASIWAZE

Nawal ndiye aliyeamua kuondoka kwenye ndoa hiyo kwa kile alichoeleza kuwa amechoka, alienda mbali zaidi na kutengeneza picha za uongo kuonyesha amefunga ndoa nyingine ili kuchora mstari kati yake na Nuh.

  1. Irene Uwoya

Ndoa na Irene Uwoya na Dogo Janja ilighubikwa na usiri mkubwa katika kufungwa kwake ingawa tetesi za wawili hao kuwa kwenye mahusiano tayari zilikuwepo.

Ndoa Mastaa Bongo

Wawili hao waliripotiwa kufunga ndoa Novemba 2017 ilipofika Septemba 2018 taarifa za kuachana kwao zikaanza kuchukua nafasi hasa kwenye mitandao ya kijamii.

Hii ilikuwa ni ndoa ya pili kwa Irene Uwoya kuvunjika ambaye hapo awali alikuwa ameolewa na mcheza soka, Hamad Ndikumana ambaye kwa sasa ni marehemu. Ndoa hii ya kwanza ilifungwa Julai 2009 katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.

  1. Steve RnB

Mwimbaji huyu wa Bongofleva aliyejikita kwenye miendoko ya RnB, alifunga ndoa na Oktoba 2014 na mpenzi wake, Naimana kwenye kanisa la Word Alive lililopo Sinza jijini Dar es Salaam.

Ndoa hii ilidumu takribani miaka mitatu, kwani ilipofika Oktoba 2018 ndipo Steve RnB aliweka wazi hayupo tena kwenye bila kueleza sababu zaidi kuacha jambo hilo kuwa la kibinafsi zaidi kati yao.

Ikumbukwe ndoa ya wawili hawa ilivuta zaidi hisia za wengi kwani wote walisoma sekondari moja na chuo kimoja, yaani Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), kisha wakaoana.

  1. Shamsa Ford

Muigizaji huyu wa filamu ndoa yake na Mfanyabiashara, Chidi Mapenzi ilidumu kwa takribani miaka mitatu, walifunga ndoa Septemba 2016 na kufikia Mei 2019 wakaachana.

Kabla ya kuachana kwao tetesi za ndoa yao kukalia kuti kavu tayari zilikuwa zimeshika kasi kwenye mitandao, ingawa wote wawili walikuwa wakikanusha vikali hilo.

Soma pia Wasanii 10 waliotazamwa zaidi YouTube Afrika!

Shamsa ndiye aliyejitokeza hadharani na kusema ndoa yao imepitiwa na jini mkata kamba, baada ya hapo, miezi kadhaa mbele Chidi akajitokeza mtandaoni kumuomba Bibie arudi nyumbani lakini ombi lake likatupiliwa mbali!.

  1. Stamina

Kabla ndoa ya Rapa huyu na mkewe kuvunjika, tayari habari za ndoa hiyo kuelekea ukingoni zilishafika mezani kwa waandishi wa udaku ingawa Stamina alikwepa kuzungumzia hilo.

Ndoa Mastaa Bongo

Walifunga ndoa Mei 2018 na ilipofika Aprili 2019 ukawa mwisho wa ndoa yao ambayo ililodumu kwa miezi 10 pekee, hawakuweza hata kusherekea mwaka mmoja wa ndoa yao.

Stamina hana kifua cha kuficha mambo aisee!, aliamua kueleza yote yaliyotokea katika ndoa yake kupitia wimbo wake, Asiwaze (2020) akieleza kujutia kufunga ndoa hiyo.

  1. Mabeste

Rapa huyu na aliyekuwa mkewe, Lisa Fickenscher walifunga ndoa Oktoba 2016 baada ya kuishi pamoja kwa muda hadi kujaliwa kupata moto mmoja.

Lisa alikuwa mwenye mchango mkubwa kwenye muziki wa Mabeste hadi kutokea kwenye video kadhaa za muziki wake, taarifa za ndoa hii kuvunjika ziliwekwa hadharani Januari 2021.

Ndoa hii iliyodumu kwa takribani miaka minne, inadaiwa moja ya sababu za kuvunjika kwake ni masuala ya fedha katika familia, huku Mabeste akieleza ilifikia wakati akataka kujitoa uhai baada ya ndoa yake kuvunjika.

  1. Shilole

Kuvunjika kwa ndoa yake ni taarifa zilizoshtua ghafla hasa pale alipoonyesha picha akiwa amepigwa na kujeruhiwa vibaya na mume wake, Uchebe.

Ndoa Mastaa Bongo

Ndoa yao ilivunjika ikiwa imedumu kwa miaka miwili na nusu, walifunga ndoa Desemba 2017 na kufikia Julai 2020 wakachana huku kila mmoja akieleza sababu inayotofautiana na mwenzake.

Baadaye ya kuachana kwao kila mmoja alionekana ndani ya penzi jipya na kutamba zaidi, huku vijembe vya hapa na pale mtandaoni vikichukua nafasi, baadaye Shilole alikuja kulewa tena na mpenzi wake wa zamani, Rommy.

Na hizi ni baadhi tu ya ndoa za Mastaa Bongo zilizokwenda na maji ila zipo nyingi.

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!