JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Wajue Mastaa Bongo waliosoma hadi Chuo na taaluma zao!

Wajue Mastaa Bongo waliosoma hadi Chuo na taaluma zao!

Kabla na baada ya kuingia katika sanaa, baadhi ya Mastaa Bongo kutoka kwenye kiwanda cha muziki na filamu alikaa darasani na kusomea taaluma ambazo wanaona zitawafaa katika maisha yao.

Mastaa Bongo taaluma

Hawa ni baadhi ya Mastaa Bongo ambao wamekaa darasani na kupata taaluma zao kuanzia gazi ya Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma), Shahada (Degree), Shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada ya Uzamivu (PhD).

Soma pia Chanzo cha utajiri wa Rihanna, Kanye West na Jay Z

  1. Wema Sepetu – International Business

Mara baada ya kukabidhi taji la Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu alienda nchini Malaysia katika chuo cha Limkokwing aliposomea Biashara ya Kimataifa (International Business), wakati akiwa chuo ndipo filamu yake ya kwanza, A Point of No Return ilipotoka na kukatisha masomo.

Mastaa Bongo taaluma
  1. Mwana FA – Finance

Awali alisomea Informationa Technology katika chuo Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kwa ngazi ya Astashahada, kisha akabadili upepo na kusomea Usimamizi wa Fedha (Finance) toka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), na baadaye alienda kujiendeleza Uingereza hadi kupata Shahada ya Uzamili.

  1. Aika Navy Kenzo – Business Administration

Mwimbaji huyu toka kundi la Navy Kenzo, ana taaluma ya Uongozi wa Biashara (Business Administration) toka Chuo cha Punjab College, India aliposomea hadi ngazi ya shahada na huko ndipo kwa mara ya kwanza alikutana mwenzake, Nahreel.

  1. Vanessa Mdee – Law

Ni mwimbaji aliyetangaza kuachana na muziki, Vanessa amesomea Sheria (Law) hadi ngazi ya shahada toka Catholic University of Easterm Africa kilichopo nchini Kenya.

Download Music: Navy Kenzo – Company

  1. Jux – Computer Science

Mkali huyo wa RnB mwaka 2017 alihitimu Chuo Kikuu cha Guangdong kilichopo Guangzhou nchini China alipokuwa anasomea Computer Science hadi ngazi ya shahada huku akiendelea na muziki.

Mastaa Bongo taaluma
  1. Master J – Electronic Engineering

Inaelezwa hakuwa anafanya vizuri darasani hadi pale familia yake ilipohamia nchini Botswana, baadaye akaenda Ulaya ambapo alifanikiwa kupata shahada ya Uhandisi wa Umeme (Electronic Engineering) toka Chuo Kikuu cha London, Uingereza mwaka 1996.

  1. Mchopanga – Art

Kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka ‘Mchopanga’ ana shahada ya masuala ya Sanaa toka Chuo Kikuu cha Bangalore nchini India.

  1. Monalisa – Mass Communication

Muigizaji huyo ambaye yupo kwenye tasnia kwa miaka zaidi ya 20, ana Stashahada ya Mass Communication aliyoipata Wilnag Media Taining College, Nairobi nchini Kenya. Aliwahi kufanya kazi EATV katika kipindi cha Bongo Movies.

  1. Billnass – Finance

Rapa huyu ana shahada ya Usimamizi wa Fedha toka Chuo cha Biashara (CBE), chuoni hapo ndipo alikutana na mchumba wake, Nandy ambaye alikatisha masomo baada ya kuibuka mshindi wa pili katika shindano la Tecno Own The Stage lilofanyika Nigeria.

  1. Nahreel – Computer Science

Akiwa kama Mwimbaji na Prodyuza mwenye mafaniko kimuziki, pia Nahreel ni mbobezi wa Computer Science, elimu aliyoipata nchini India katika Chuo cha Punjab College alipohitimu mwaka 2011 katika ngazi ya shahada.

  1. Feza Kessy – Business Management

Kabla ya kuingia kwenye muziki, Feza alishinda Miss Dar City Centre 2005 na kushiriki Big Brother Africa (BBA) 2013, ana Stashahada ya Information Technology (IT), pia ana shahada ya Usimamizi wa Biashara (Business Management) aliyoipata Uingereza.

  1. Roma – Computer Science

Mkali huyu wa michano toka kundi la Rostam anayeishi Marekani sasa, naye ni mtaalamu wa Computer Science toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alipohitimu ngazi ya shahada mwaka 2012.

Mastaa Bongo taaluma
  1. Mimi Mars – Law

Staa huyu wa Bongofleva na filamu, kwanza alisoma St. Catherine Mountain View, Nairobi nchini Kenya. Ana Shahada ya Sheria toka Kampala University, pia amesomea Tourism Management toka Malaysia Nilai University.

  1. Nikki wa Pili – Development Studies

Rapa huyu toka kundi la Weusi ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya, ana Shahada ya Uzamili upande wa maendeleo
toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), mwaka 2014 alitangaza kurudi shule ili kutimiza ndoto yake ya kupata Shahada ya Uzamivu.

  1. Lady Jaydee – Journalism

Mwimbaji huyu amewahi kusomea Uandishi wa Habari katika Chuo cha TIME School of Journalism (TSJ), Dar es Salaam katika ngazi ya Astashahada, kisha akafanya kazi na Clouds FM Radio kwa kipindi kifupi na baadaye kuja kuandika historia ndani ya Bongofleva.

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!