JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Maria (Mimi Mars) aondolewa Jua Kali, nafasi yake apewa Lulu

Maria (Mimi Mars) aondolewa Jua Kali, nafasi yake apewa Lulu

Muigizaji Maria (Mimi Mars) ameondolewa katika thamthilia ya Jua Kali na nafasi yake imechukuliwa na Elizabeth ‘Lulu’ Michael ambaye tayari ameanza kazi.

Maria Jua Kali

Mtayarishaji wa tamthilia hiyo, Lamata kupitia ukurasa wake wa Instagram ndiye ametoa taarifa hiyo ambayo imewashtua mashabiki wake ambao walikuwa wanatarajia Maria kurejea hivi karibuni baada ya kupata ajali.

Soma pia Mkate mkubwa wa Mimi Mars upo kwa Maria

Utakumbuka Maria alikuwa nje ya Jua Kali kwa muda baada ya kupata ajali na hivi majuzi katangaza kupona ikiwa ni taarifa njema kwa mashabiki wake na tamthilia ya Jua Kali ila imekuwa ndivyo sivyo.

Maria Jua Kali

Chini tumenukuu ujumbe wa Lamata.

Chaneli ya Maisha Magic Bongo (MMB), inawataarifu watazamaji na wapenzi wa tamthilia ya Jua Kali kuwa, kutokana na sababu zisizozuilika na baada ya majadiliano na wahusika, imefikia uamuzi wa kumbadilisha muigizaji aliyekua akicheza uhusika wa Maria (Marianne Mdee) Mimi Mars na kwa sasa, Elizabeth Michael (Lulu) anavaa uhusika huo.

MMB inapenda kutoa shukrani za dhati kwa Marianne, kwa mchango wake katika tasnia hususani uhusika wake mkuu katika Jua Kali.

Karibu sana Elizabeth, katika boma la DStv.

Usikose kufuatilia Jua Kali kila Jumatano hadi Jumapili saa 03:30 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo, (DStv 160).

Download Music: Mimi Mars Ft. Darassa – Give Up

Ikumbuwe Maria aliwahi kushinda tuzo ya Tanzania Film Festival Awards 2021 kama Muigizaji Bora wa Kike Chaguo la Watazamaji, huku tamthilia ya Juakali ikiondoka na tuzo nne.

Pia alishinda tuzo kutoka The Orange Awards 2023 kama Muigizaji Bora wa Kike wa Mwaka baada ya kuwabwaga wenzake kama Jenifa Kanumba (Huba), Lulu Diva (Juakali), Nelly Kamwelu (Huba) na Dorah (Juakali).

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!