JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Maria (Mimi Mars) ataja sababu ya kuondoka Jua Kali

Maria (Mimi Mars) ataja sababu ya kuondoka Jua Kali

Hatimaye muigizaji Maria (Mimi Mars) ametaja sababu ya kuondoka katika tamthilia ya Jua Kali kitu ambacho kimezua mjadala mkubwa kutoka kwa mashabiki wake na wapenzi wa mchezo huo.

Siku chache zilizopita Mtayarishaji wa tamthilia ya Jua Kali, Lamata alitoa taarifa kuwa Maria (Mimi Mars) ameondolewa katika thamthilia hiyo na nafasi yake imechukuliwa na Elizabeth ‘Lulu’ Michael.

Soma pia Maria (Mimi Mars) aondolewa Jua Kali, nafasi yake apewa Lulu

Katika video aliyoichapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Maria amesema baada ya kupata ajali ya gari aliumia kichwani, hivyo Daktari akamshauri asifanye kazi kwa muda mrefu ili kupata muda zaidi wa kupona.

Mimi Mars Jua Kali

“Naendelea kupona taratibu, kwa hiyo katika vitu ambavyo nilishauriwa, nisifanye kazi ambayo inatumia nguvu nyingi na muda mwingi sana ikiwemo uigizaji, kwa hiyo muda huo kwa sasa baado sijapewa,” amesema.

“Nimeruhusiwa kurudi kwenye muziki, u-MC na utangazaji wa bidhaa nyingine lakini kwenye uigizaji bado, kwa hiyo Jua Kali kama wangenisubiria nifike, wangewaharibia stori kabisa,” amesema.

“Nashukuru sana kwamba ameweza kupatikana mtu mwingine wa kucheza nafasi ya Maria na mmeweza kuendelea na Jua Kali. Nawashukuru sana, nawapenda sana, tutaonana katika tamthilia nyingine,” amesema Mimi Mars.

Awali taarifa ya Lamata aliyoitoa Aprili 2024 kukupitia ukurasa wake wa Instagram ilisomeā€¦.

Chaneli ya Maisha Magic Bongo (MMB), inawataarifu watazamaji na wapenzi wa tamthilia ya Jua Kali kuwa, kutokana na sababu zisizozuilika na baada ya majadiliano na wahusika, imefikia uamuzi wa kumbadilisha muigizaji aliyekua akicheza uhusika wa Maria (Marianne Mdee) Mimi Mars na kwa sasa, Elizabeth Michael (Lulu) anavaa uhusika huo.

MMB inapenda kutoa shukrani za dhati kwa Marianne, kwa mchango wake katika tasnia hususani uhusika wake mkuu katika Jua Kali.

Ikumbuwe Maria aliwahi kushinda tuzo ya Tanzania Film Festival Awards 2021 kama Muigizaji Bora wa Kike Chaguo la Watazamaji, huku tamthilia ya Juakali ikiondoka na tuzo nne.

Pia alishinda tuzo kutoka The Orange Awards 2023 kama Muigizaji Bora wa Kike wa Mwaka baada ya kuwabwaga wenzake kama Jenifa Kanumba (Huba), Lulu Diva (Juakali), Nelly Kamwelu (Huba) na Dorah (Juakali).

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!