JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Huyu Alikiba ana misimamo mikali sana, hakuna cha kumbabaisha!

Huyu Alikiba ana misimamo mikali sana, hakuna cha kumbabaisha!

Mwimbaji wa Bongofleva kutokea Kings Music, Alikiba anazidi kuonyesha misimamo kwa baadhi ya mitindo inayoibuka na kuvuma katika tasnia jambo linalomfanya kuishi katika dunia yake ukilinganisha na wasanii wengine.

Alikiba misimamo

Alikiba aliyetoka kimuziki chini ya G Records ameshatoa albamu tatu, Cinderella (2007), Ali K4Real (2009) na Only One King (2021), huku akishinda tuzo za TMA, MTV, Afrimma, Sound City, BEFFTA na aliwahi kusainiwa Sony Music Africa.

Soma pia Biashara hadi ugomvi kati ya Diamond na Harmonize!

Misimamo ya Alikiba utaiona kwa jinsi anavyofanya muziki na kuendesha lebo yake ya Kings Music na mtindo wake wa maisha ambao kwa asilimia kubwa una uhusiano na kazi yake ya muziki.

Alikiba misimamo

Hata upepo mkali wa muziki wa Singeli ulipovuma na kuwachukua wasanii wa Bongofleva kama Harmonize, Zuchu, Ben Pol, Ommy Dimpoz, Marioo n.k, Alikiba alitunisha misuli kwa misimamo, hakuchukuliwa na upepo huo!.

Kipindi wasanii wake wawili, Cheed na Killy wanaondoka Kings Music, Alikiba aliwatakiwa kila la heri huko waendako, alidai hakuwa na mikataba nao kwani Kings Music ni kama Chuo cha muziki, watu wanajifunza na wanaweza kuondoka.

Huu ni zaidi ya ujeuri, lebo inawezaje kuwekeza kwa msanii bila mkataba, hata walivyoondoka ilikuwa kiwepesi sana, kulikuwa hakuna kitu cha kuwafunga, hiyo ni tofauti na baadhi ya lebo Bongo ambazo msanii akitaka kuondoka lazima moto uwake!.

Ila kilichokuja kuwakuta Cheed na Killy baada ya kuachwa na Konde Music ya Harmonize, ndio utajua Alikiba ana ujeuri, ni kama alijua hawatofika mbali hivyo hakuna na sababu ya kuangaika nao.

Utakumbuka wakati Alikiba anatambulishwa kama Mkurugenzi wa RockStar Africa na kumsaini Ommy Dimpoz, ghafla Barakah The Prince alijiondoa katika Menejimenti hiyo, Alikiba akasema kama ameamua hivyo, acha dunia ikamfunze, leo hii Barakah yupo wapi?.

Halafu Alikiba ana misimamo ya kufanya muziki wake kwa lugha inayofaa, hakuna wimbo wake wala video yake ambavyo imewahi kufungiwa kwa kukiuka maadili, muziki wake unasikilizika na kila rika na bado unafanya vizuri.

Wakati wasanii kibao wakijipachika majina ya wanyama wakali wa mwituni kama sehemu ya kuonyesha ukali wao katika muziki, Alikiba hana jina la myama, aliwahi kusema yeye ni Mfalme hivyo wanyama wote wapo chini yake!.

Alikiba misimamo

Baadhi ya wasanii waliojipachika majina ya wanyama ni Diamond (Simba), Harmonize (Tembo), Rayvannny (Chui), Country Boy (Fisi), Dubu Baya (Mamba), Afande Sele (Simba Dume), Mr. Blue Nyani Mzee nk.

Ukitazama ukurasa wake wa Instagram ambao una wafuasi (followers) milioni 9, Alikiba hajamfuta (follow) mtu hata mmoja, hiyo ni sawa na Beyonce Knowles, mke wa Jay Z ambaye ana wafuasi milioni 312, King Kiba na Queen B wote wajeuri tu!.

Download Music: Alikiba – Mahaba

Katika mahojiano yake na Podcast ya Swahili Radio by Audiomack Africa hapo , Alikiba alisema kuwa kama ikitokea akaanza kuwafuta (follow) watu Instagram, basi ataanza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Utakumbuka kuna wakati mtandao wa Instagram ulipunguza wafuasi kwa watu wajeuri kama Alikiba ambao hawataki kuwafuata wenzao, ila hilo halikumtisha Alikiba, hadi leo ametia ngumu. Anaamini kufanya hivyo kutamfanya kumjua shabiki yake wa kweli ni yupi!.

Katika nyakati hizi ambazo wasanii wamechafua miili yao kwa kuchora tattoo za kila namna kama za wazazi wao, wapenzi na matukio mabaya au mazuri yaliyowahi kuwatokea, Alikiba alipitiwa mbali na upepo huo, ana ujeuri tu wa kufanya muziki na ukapendwa sio lazima awe na tatttoo!.

Mwimbaji Shilole aliwahi kueleza kuwa miongoni mwa mambo anayojutia katika yake ya muziki ni kuchora tattoo katika mwili wake, naye Mh. Temba aliwahi kuondolewa JKT kutokana amechora tu tattoo mwilini.

Alikiba misimamo

Na hadi sasa wasanii kibao Bongo wamefanya video na wapenzi wao na hata wake zao kitu ambacho ni kizuri kwani huvutia zaidi na kuleta uhalisia, ila Alikiba hajawahi kujaribu jambo hilo, ni ujeuri wake tu.

Utakumbuka baadhi ya wasaniii Bongo waliofanya hivyo ni Diamond (Wema Sepetu, Zari The Bosslady na Hamisa Mobetto), Harmonize (Jacqueline Wolper, Sarah na Kajala Masanja), Rayvanny (Fahyma na Paula), Mabeste (Lisa Fickenscher), Barnaba (Zuu au Mama Steve), Marioo (Paula), Jux (Vanessa Mdee na Nayika) n.k.

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!