JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Historia ya Jay Melody kimuziki

Historia ya Jay Melody kimuziki

Kwa mujibu wa historia ya Jay Melody kimuziki huko nyuma, inasema kwa sasa yupo katika kilele cha mafanikio ya kazi yake ya muziki baada ya kupotea na hata kusahaulika ila akarejea na kufanya vizuri kuliko mwanzo.

Historia ya Jay Melody

Huyu aliwahi kunolewa pale Tanzania House of Talent (THT) alipotoka kimuziki na wimbo wake, Goroka (2018), zilifuata nyimbo nyingine mbili zilizofanya vizuri ambazo ni ‘Namwaga Mboga’ ft. Nandy na ‘Mikogo Sio’ ft. Dogo Janja.

Soma pia: Historia ya Rayvanny kimuziki

Baada ya hapo nyimbo alizotoa hazikufanya vizuri na kufuatia kifo cha Ruge Mutahaba (2019), mwalimu, msimamizi wake kimuziki pale THT na mtu aliyempa jina la “Jay Melody”, wengi wakaamini hatoweza kuja kuwika tena kimuziki.

Ni kweli alipotea, mfano nyimbo zake tatu za mwanzo video zake zilifikisha ‘views’ zaidi ya milioni 1 YouTube, video ya wimbo, ‘Namwaga Mboga’ ndio ilifanya vizuri zaidi hadi sasa ikiwa na ‘views’ milioni 2.5, ila baada ya hapo hakuweza kufikia tena mafanikio hayo.

Katika moja ya mahojiano yake, Jay Melody anakiri hali ilikuwa mbaya kwake kimuziki hadi kufikia hatua ya kwenda kwa mganga na kuishi kabisa huko ili kutazama nyota yake na kujua kwanini hafanyi vizuri kama alivyoanza.

Januari 2021 aliachia wimbo wake, Huba Hulu ambao umechukua vionjo kutoka katika wimbo, El Habayib wake Amr Diab, Huba Hulu akawa wimbo mkubwa kila kona, kuna ambao ndio walimjua Jay Melody kwa mara ya kwanza kupitia wimbo huo.

Historia ya Jay Melody

Huba Hulu ulifanya vizuri kuliko ‘Goroka’ na ‘Namwaga Mboga’, hadi sasa video yake ina ‘views’ zaidi milioni 3.5 YouTube, gari likawa limewaka upya kwa Jay, zikafuata ngoma nyingine kali kama Najiweka na Sugar ambayo video yake ina ‘views’ milioni 14 hadi sasa.

Wimbo wake, Nakupenda uliotoka Julai 2022 akazima mitaa yote, ndio wimbo pekee wa Bongofleva uliofanya vizuri zaidi katika majukwaa yote ya kidigitali ya kusikiliza muziki kwa mwaka 2022.

Hadi sasa ‘Nakupenda’ ndio wimbo wa Bongofleva uliosikilizwa zaidi Boomplay kwa muda wote ukiwa na ‘streams’ milioni 79.8, baada ya hapo aliachia nyimbo nyingine kama ‘Acha Wivu’ ‘Nitasema’ na ‘Sawa’ ambao umefikisha ‘streams’ milioni 35.3.

Historia ya Jay Melody

Kwa mujibu wa Jay Melody kwa miezi mitatu tangu ulipotoka wimbo, Sugar ulimuingizia Sh30 milioni, na kupitia wimbo, Nakupenda ametengeneza zaidi ya Sh200 milioni kutokana na show na mauzo mtandaoni.

Utakumbuka ‘Nakupenda’ ni wimbo uliopatia tuzo ya muziki Tanzania (TMA) 2022 kama Wimbo Bora wa Mwaka ikiwa ni tuzo yake ya kwanza kushinda Bongo tangu ameanza muziki mwaka 2016.

Download Music: Diamond Platnumz ft. Mr. Blue & Jay Melody – Mapoz

Ni ushindi uliokuja miaka miwili baada ya kurejea tena katika muziki na kuifanya historia ya Jay Melody kimuziki kuwa kubwa zaidi.

Na mwishoni mwa 2023 Jay Melody alifikisha ‘streams’ milioni 200 Boomplay na kuandika rekodi kama msanii wa kwanza wa Bongofleva kufanya hivyo bila kuwa na albamu wala EP kama wasanii wengine.

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!