JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Yajue mapito ya Rich Mavoko baada ya kuondoka WCB Wasafi

Yajue mapito ya Rich Mavoko baada ya kuondoka WCB Wasafi

Ni miaka minne sasa tangu mwimbaji wa Bongofleva, Rich Mavoko kuachana na WCB Wasafi akiwa ni msanii wa kwanza kufanya hivyo katika historia ya rekodi lebo hiyo yake Diamond Platnumz.

Rich Mavoko WCB

Rich Mavoko alijiunga WCB Wasafi mwaka 2016 akiwa ni msanii wa tatu baada ya Harmonize na Rayvanny, aliondoa katika lebo hiyo mwaka 2018 kwa mvutano mkubwa hadi kufikishana Baraza la Sanaa Taifa (Basata).

Soma pia Utafiti: Harmonize anapenda wanawake wenye shepu!

Tofauti na wenzake, Harmonize na Rayvanny, Rich Mavoko alijiunga WCB Wasafi akiwa tayari ni msanii mkubwa aliyetamba na nyimbo kali kama Silali, Marry Me, Follow Me, Pacha Wangu, One Time n.k.

Huyu alikuwa anashindanishwa na Diamond kimuziki na ndio hata sababu kipindi anataka kuondoka yalizuka madai kuwa kusainiwa kwake WCB Wasafi ulikuwa ni mpango wa kumuua kimuziki kitu ambacho kilikanushwa na lebo hiyo.

Hata hivyo, kabla ya Rich Mavoko kusaini hakuwahi kukutana au kuongea na Diamond kuhusu hilo, AYndiye aliyemkutanisha na Sallam SK wakiwa nchini Uganda kwenye show ya Jose Chameleone ndipo yalipoanzia mazungumzo ya kujiunga.

Akiwa WCB Wasafi Mavoko alitoa nyimbo maarufu kama Ibaki Stori, Kokoro ft. Diamond Platnumz, Rudi ft. Patoranking n.k, huku akishirikishwa na Harmonize katika wimbo wake, Show Me.

Rich Mavoko WCB

Kwa mujibu wa Rich Mavoko, yeye hakulipa fedha kuondoka WCB Wasafi kama walivyofanya Harmonize na Rayvanny, ushihidi wa kimazingira unaweza kuthibitisha hilo kwa kutazama jambo hilo moja;.

Video zote za nyimbo ambazo Rich Mavoko alizotoa chini ya WCB Wasafi kama Ibaki Stori, Kokoro, Rudi n.k, zimeondolewa katiika mtandao wa YouTube, huku chaneli yake iliyokuwa na video hizo na zake nyingine za hapo awali ikiwa haitumiki tangu kuondoka kwake.

Inawezekena chaneli hiyo ilibaki chini ya WCB Wasafi na ndio sababu ya kwenda kuanzisha nyingine, Billionea Kid hapo Agosti 14, 2018 ambayo hadi sasa imefikisha ‘views’ milioni 17.4.

Tangu kuachana na WCB Wasafi video za nyimbo zake zilizofanya vizuri zaidi YouTube ni Naopoga ‘views’ milioni 2.1, Mapenzi – milioni 1.5, Wamoto – milioni 1.5, Ndegele – milioni 1.3 na Niwahi – milioni 1.2.

Download Music: Rich Mavoko Ft. Fid Q – Blow Up

Hiyo ni tofauti kabisa kwa Harmonize na Rayvanny ambao waliondoka na chaneli zao baada ya kulipa kile kinachoitwa fidia ya mkataba, hawa wamekuwa wakipata namba za juu zaidi. Hili linatoa picha kuwa njia aliyochagua Rich Mavoko kuanza upya pengine ilikuwa ni ngumu zaidi kwake.

Ikumbukwe wimbo wake wa kwanza kutoa baada ya kuachana na WCB Wasafi ni ‘Ndegele’ uliotoka Agosti 17, 2018, video yake iliyoongozwa na Director Adam Juma hadi sasa ina ‘views’ milioni 1.2.

Rich Mavoko WCB

Mwaka 2023 Mavoko alikaa wiki 26, yaani zaidi ya miezi sita bila kuchapisha chochote katika mitandao yake ya kijamii, wakati wasanii wengine wakipambana kutengeneza maudhui ya kuvutia mtandao ili kupata dili mbalimbali kama za ubalozi, Mavoko yeye kaipa kisogo mitandao.

Pengine alikuwa anajiandaa kuachia kazi mpya tangu kufanya hivyo Novemba 27, 2022 alipoachia wimbo wake, Stamina, lakini mbona kuna wasanii kama Alikiba, Nandy, Ommy Dimpoz n.k huchukua hata miezi sita bila kutoa kazi ila huendelea kuwepo mitandaoni?.

Rich Mavoko WCB

Hii sio mara ya ya kwanza kufanya hivyo, kipindi anajiandaa kuachia Minitape (2020) na albamu yake, Fundi (2022), napo alipotea mitandaoni ndipo akaja na kazi hizo. Ukimya huu unamfanya Mavoko kutozungumziwa sana, hilo linaathiri hata pale anapotoa kazi zake mapokezi yanakuwa sio makubwa sana.

Kuna wasanii wengi wakubwa Bongo waliofanikiwa na wanafanya vizuri kwa sasa, lakini huwezi kuamini huwa wanalipa fedha ili kuandika kivyovyote kwenye mitandao na hata kujadiliwa kwenye kurasa za udaku, wanajua hapo ndipo inapotokea nguvu yao, ila Rich Mavoko kaamua kujiweka kando na mitandao.

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!