JamboMail.com – Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle

The most read Swahili entertainment website in Tanzania, East Africa.

Nyimbo alizoimbiwa Ray C akisifiwa kisa “kiuno bila mfupa”

Nyimbo alizoimbiwa Ray C akisifiwa kisa “kiuno bila mfupa”

Hakuna ubishi kuwa Ray C ni mwimbaji aliyebarikiwa sauti ya kusisimua na nyimbo zake nzuri na mahiri kuhusu mapenzi ila ‘kiuno bila mfupa’ kiliwakosha wengi.

Ray C kiuno

Ray C ni mshindi mara mbili wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) kama Msanii Bora wa Kike kwa mwaka 2004 na 2007, huku akiwa ametoa albamu moja, Mapenzi Yangu (2003).

Ray C kiuno

Hata hivyo, mbali na uimbaji wake, Ray C amekuwa akipewa sana sifa kutokana na uchezaji wake uliopelekea kupewa jina la kiuno bila mfupa, sio kwa mashabiki tu, ni wasanii wengi Bongo katika nyimbo zao wamempa Ray C sifa hiyo kama ifuatavyo;

  1. Mwana FA – Mabinti (2002)

Rapa huyu ambaye sasa ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, kupitia wimbo wake, Mabinti amewarusha warembo kibao na mmoja wapo ni Ray C na kumpa sifa yake ya kipekee inayotambulika na wengi.

“Una kifua kama cha Zay B, kiuno kama cha Ray C, na pozi kama za Jay Dee na sauti kama Fina.” Mwana FA katika ngoma, Mabinti kutoka katika albamu yake ya kwanza, Mwanafalsafani (2002).

Soma pia Nyimbo 10 alizoimbiwa Wema Sepetu

Utakumbuka Mwana FA, Ray C na Banana Zorro walishirikishwa na AY katika wimbo wake, Safi Hiyo uiliotengenezwa na Prodyuza Xosa kutoka Backyard Records, ngoma hiyo ni kutoka katika albamu ya kwanza ya AY, Raha Kamili (2003).

  1. Fid Q – Kadi na Ua Rose (2005)

Nguli huyu wa Hip Hop katika albamu yake ya kwanza tu, Vina Mwanzo Kati na Mwisho (2005) aliamua kumsifia kwanza Ray C kupitia wimbo wake, Kadi na Ua Rose akimshirikisha Lady Jaydee.

Ray C kiuno

“Sauti yako inanivutia kama vinanda vya Majani, hauna tu jina kubwa kama la Lady Jaydee, lakini una kiuno bila mfupa kama Ray C.” Fid Q katika ngoma, Kadi na Ua Rose au Goodnite.

Ikumbukwe ‘Kadi na Ua Rose’ ni miongoni mwa nyimbo za mwanzo kabisa za Fid Q kuhusu mapenzi kisha zikafuta nyingine kama Usikunikubali Haraka na Danger zote kutoka katika albamu yake ya pili, Propaganda (2009).

  1. Mangwair – Speed 120 (2010)

Ni wimbo wa kwanza kutoka katika albamu yake ya pili, NG’E 1982 (2010) alimshirikisha Chid Benzi, huku Kama Kawa Records ikuhusika, humu Mangwair alimrusha Ray C katika ‘verse’ ya kwanza tu.

“Usishangae nisipopanda na masteji shoo, waulize hao mabitozi kujipodoa hawaoni soo. Mwishoni wataka viuno stejini kama Ray C, au watakuja kuiga hata ‘diary’ za Lady Jaydee.” Mangwair katika ngoma, Speed 120.

Utakumbuka Mangwair aliyefariki mwaka 2013 nchini Afrika Kusini, katika maisha yake ya muziki alitoa albamu mbili, A.K. A Mimi (2004) na NG’E 1982 (2010).

  1. Young Killer – Mrs SuperStar (2013)

Baada ya kuachia ngoma, Dear Gambe iliyotambulisha vizuri, Young Killer alirudi kwa mashabiki wake ngoma, Mrs SuperStar ambayo alielezea mastaa wa kike Bongo ambao anatamani kuwa nao ila kuna kuwa na changamoto, mmoja wapo alikuwa ni Ray C.

“Ama Ray C nikimcheki machoni haishi, kile kiuno bila mfupa kingenipikia mapishi. Ila ghafla nikaogopa niliposikia ana mchizi, baada ya kuuliza ni nani kumbe mnako Lord Eyes.” Young Killer katika ngoma, Mrs SuperStar akiwashirikisha Bright na Nemo.

Ikumbukwe kufanya vizuri kwa ngoma hizo mbili ndipo kulipelekea Young Killer kushinda tuzo yake ya kwanza ya KTMA 2014 kama Msanii Bora Chipukizi akipokea kijiti kutoka kwa Ally Nipishe aliyeshinda mwaka 2013.

  1. Harmonize – Uno (2019)

Staa huyo wa Konde Music Worldwide alimrusha Ray C katika ngoma yake, Uno ambayo ilikuwa ya kwanza kuachia baada ya kuachana rasmi na WCB Wasafi, Ray C alionyesha kuheshimu hiki alichofanya Konde Boy.

Ray C kiuno

“Uno la Ray C halinaga mifupa, ukienda DRC kuna Fally Ipupa.” anaimba Harmonize katika ngoma, Uno iliyokuja kuwekwa katika albamu yake ya kwanza, Afro Bongo (2020).

Download Music: Zuchu – Napambana

Utakumbuka miongoni mwa wasanii wa miaka ya hivi karibuni waliobahatika kufanya kazi na Ray C, ni Rayvanny, rais wa Next Level Music (NLM) ambaye amemshirikisha katika wimbo wake, Honey kutoka katika EP yake ya pili, Flowers II (2022).

Editor

Related Posts

Lifahamu tamasha la Met Gala

Lifahamu tamasha la Met Gala

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Billnass afunguka kwanini hajataka kuajiriwa

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Diamond, DJ Khaled waiga maujanja ya Madee

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

Mkasa wa Hamisa Mobetto kutoswa na Diamond studio

error: Content is protected !!